Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hassan Hanizadeh, mchambuzi wa masuala ya kisiasa, katika mazungumzo na mwandishi wa shirika la habari la Hawza mjini Tehran, huku akirejelea mabadiliko ya msimamo wa rais wa Ufaransa kuhusu kupelekwa kwa meli ya kubeba ndege ya kivita “Charles de Gaulle” katika eneo hilo na Ghuba ya Uajemi alisema: “Tangazo la awali la Emmanuel Macron kuhusu kupeleka meli hiyo lilikuwa kwa lengo la kufungua Mlango wa Hormuz, lakini lilikabiliwa na radi amali na onyo kali kutoka Iran kupitia taasisi ya diplomasia na vikosi vya jeshi.”
Aliongeza: “Hapo kabla pia Marekani ilikuwa imejaribu hatua kama hiyo kwa kupeleka manowari za kivita zikiwemo USS Gerald R. Ford, USS Abraham Lincoln na USS George H. W. Bush katika eneo hilo, lakini haikufikia matokeo yaliyotarajiwa. Suala la uwepo wa manowari za kijeshi za mataifa ya Magharibi katika eneo hili si jambo jipya, lakini Iran kupitia nguvu zake za kijeshi na kisiasa imeweza kuunda uwezo madhubuti wa kuzuia.”
Mchambuzi huyo wa kisiasa, huku akirejelea hatua ya hivi karibuni ya Ufaransa kurudi nyuma, alisema: “Mabadiliko haya ya msimamo yanaonyesha kuwepo mpasuko na mfumo wa pande nyingi kati ya nchi za Ulaya na Marekani, na yanaonesha kwamba; Iran ina nguvu kubwa ya kufanya mazungumzo na kuunda mjadala wa kikanda.”
Hanizadeh alisisitiza: “Ufaransa katika kipindi cha sasa kwa kiasi fulani imejitenga na njia ya Marekani, na jambo hili linaweza kuwa mwanzo wa hatua mpya katika mahusiano kati ya Iran na Umoja wa Ulaya; hususan kati ya Iran na Ufaransa ambazo hata zamani katika baadhi ya vipindi zilikuwa na misimamo tofauti na sera za Marekani.”
Aliendelea kusema: “Kurudi nyuma kwa Emmanuel Macron kuhusu kupeleka manowari ya kivita kunaweza kuwa ishara chanya ya kupungua kwa mvutano na kuandaliwa mazingira ya maingiliano yenye kujenga zaidi kati ya Iran na nchi za Magharibi.”
Mchambuzi huyo akiashiria athari za mwelekeo huo kwa sera ya nje ya Ulaya katika eneo la Ghuba ya Uajemi alisema: “Nguvu ya Iran katika nyanja ya kijeshi na kiusalama ndani ya Ghuba ya Uajemi na Mlango wa Hormuz iko wazi kabisa, na jambo hili limekuwa na athari katika hesabu za kikanda.”
Akirejelea kushindwa kwa sera za Marekani na utawala wa Kizayuni katika kubadilisha mlinganyo wa eneo hilo, aliongeza: “Mkusanyiko wa matukio ya hivi karibuni, ikiwemo kushindwa kwa kijeshi na kiusalama katika eneo hili, umefanya baadhi ya nchi za Ulaya kupitia upya sera zao na kuchukua njia huru zaidi ikilinganishwa na Marekani.”
Hanizadeh alisisitiza kuwa: “Hali hii inaweza kuandaa mazingira ya kupungua kwa mvutano na kuongezeka kwa kujenga uaminifu katika eneo hili, hususan katika Mlango wa Hormuz.”
Katika kuendelea, kuhusu ukweli wa misimamo ya hivi karibuni ya rais wa Ufaransa alisema: “Inapaswa kuonekana katika siku zijazo iwapo Emmanuel Macron atabaki mwaminifu kwa kauli zake au la. Kwa hali yoyote, Ufaransa kama nguvu ya Ulaya inapaswa kuwa na mtazamo wa kuwajibika kuhusu mabadiliko ya kikanda, kwa sababu inaweza kuiletea madhara makubwa zaidi nchi hiyo yenyewe.”
Mchambuzi huyo wa masuala ya kisiasa mwishoni alisema: “Uzoefu umeonesha kuwa Ufaransa ikilinganishwa na baadhi ya nchi za Magharibi ina sera yenye msimamo wa wastani zaidi kuhusu eneo la Asia Magharibi, na inajaribu kuhifadhi mahusiano yake na nchi za Kiislamu pamoja na Iran ndani ya mfumo unaozingatia maslahi ya pamoja.”
Maoni yako